Wednesday, August 14, 2013

WATANZANIA TUMLINDE MWAKYEMBE MUNGU ANAKUSUDI NAYE KWETU

Kwamala nyingine tena wazili wa Uchukuzi Mh Dr. Harrison Mwakyembe a.ka JEMBE amevunja ukimya kwa kuamua kuchukua uamzi mgumu wa kushughurika na wauzaji wa madawa ya kulevya nchini. Mwakyembe ametoa siku 14 kuanzia jana na akaahidi kuwashughurikia kwa udi na uvumba watu wanaofanya biashara ya kuingiza na kuuza unga nchini. Akionyesha uwajibikaji leo Mwakyembe amefanya ziara ya kushitukiza katika uwanja wa ndege wa Mwalim J.K Nyerere ili kuongea na wafanyakazi na kujua nini kifanyike.

Mwakyembe amekua kiongozi wa mfano kwa kutofumbia macho maovu ambayo yanafanyika katika wizara yake katika kipindi chote ambacho amekua waziri. Itakumbukwa kuwa toka ateuliwe kuwa waziri wa uchukuzi mwakembe ameweza kushughurika na tatizo sugu katika bandari ya Dar es Salaam na kuondoa uozo na mizizi ya baadhi ya watumishi ambao walikuwa ni kikwazo cha ufanisi na utendaji kazi bandarini hapo. Tokea yafuanyike malekebisho hayo mapato ya bandari yameongezeka sanjari na ufanisi umeimalika kiasi cha kurudisha imani kwa watumiaji wa bandari hiyo.

                                          Waziri wa Uchukuzi DR. Harrison Mwakyembe

Wito wangu kwa watanzania wa dini zote na wasiokuwa na dini kumuombea Dr. Mwakyembe katika utendaji wake wa kazi hasa pale anapofanya kazi kwa masrahi ya taifa. Itakumbukwa kuwa viongozi wengi wameshindwa kupambana na vita hii kufuatia uwezo wa kifedha wa watu wanaofanya biashara hiyo kwa kuwa tayari kufanya lolote. Watanzania wenzangu ifike hatua tutambue kuwa ulinzi wa viongozi wawajibikaji uko mikononi mwetu hivyo ni vema tukajitoa muhanga kuwapigania kwa hari na mali.

Ni matumaini yangu kuwa tutampa ushirikiano wa kutosha muheshimiwa Mwakyembe katika kulisafisha taifa letu ambapo kwa sasa Tanzania imekuwa kinara wa uuzaji na usambazaji wa madawa ya kulevya. Sio hivyo tu pia inasadikika kuwa tayari mtambo wa kutengeneza dawa hizo upo nchini. Hongera sana Mwakyembe kwa kujitolea kumfunga paka kengele tuko nyuma yako.

No comments:

Post a Comment


Welcome to Youth Voice!

Follow this blog to hear from many different people every month. The youth of the world will send their views on politics, economics, society, the environment...anything! Tell us about what you've seen in the world. Tell us what you've heard. This blog will be for the youth to tell their stories from Alaska to Zanzibar!