Friday, March 29, 2013

Muuwaji wa Padri Mushi Akamatwa



Jeshi la polisi Zanzibar linamshikilia mtu mmoja alietambulika kwa jina la Omar Mussa Makame kwa tuhuma za mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar yaliotokea  mwezi uliopita. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumekuja baada ya kutolewa kwa picha yenye sura ya mtuhumiwa iliyochorwa na askari wa shirika la upelelezi la Marekani FBI.

Mtuhumiwa Omar Mussa Makame ambae ni mkazi wa  Mtaa wa Raha Leo mjini Zanzibar alikamatwa na kufanyiwa gwalide la utangulizi ambalo lilihusisha watu baadhi ambao walikuwepo siku ya tukio ambao walitambua sura ya mtuhumiwa. 

Akifafanua zaidi kamishina Mussa Ali Mussa alisema kuwa jeshi la polisi litampatia zawadi ya million kumi kwa siri mtu aliefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kama ilivyoahidi. Padri Evarist Mushi aliuwawa Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada katika kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Raas mjini Zanzibar.

 Taswira ya mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Mushi kama ilivyoandaliwa na FBI

Gari la marehemu Padri Mushi muda mfupi baada ya ya kuuwawa kwa kupigwa risasi

Gorofa laanguka Dar es salaam

Leo wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameianza siku kwa majonzi makubwa baada ya taarifa za kuanguka kwa jengo la gorofa 16 katika eneo maarufu kwa msongamano wa watu na pilika pilika mbalimbali la kariakoo. Taarifa za awali zimemkariri Meya wa Ilala mheshimiwa Jerry Silaa kuwa maiti 2 zimepatikana na majeruhi 17. Pia muheshimiwa Silaa ameeleza kuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kusimamia zoezi la uokoaji na ulinzi wa mali za raia katika eneo hilo. YOUTH VOICE inaahidi kuwaletea habari kamili kadri zitakavyo kuwa zimapatikana na kuthibitiswa na vyombo vyenye mamlaka ya kutoa taarifa.

Tunapenda kutoa pole kwa watanzania wenzetu ambao wamewapoteza ndugu na marafiki zao, pia na wale waliopata majeraha wapone haraka. Pia tunaomba zoezi la uokoaji lifanyike kwa kasi na kwa uangalifu wa hari ya juu ili kuepusha madhara kwa watu ambao wanasadikika pengine wamefukiwa na kifusi hicho. Pia tunaomba hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote ambao kwa namna moja ama nyingine walikwepa majukumu yao ama kwa kukusudia au kuto kukusudia na kusababisha jengo hilo kupolomoka. Tumechosha na hii tabia ya vifo kwa watanzania wasio kuwa na hatia ambavyo husababiswa na uzembe wa watu katika majukukmu yao




                           


                                       


Thursday, March 28, 2013

I'm back get prepared



Dear all
I’m sorry I have been out of response for almost five years this is due to many works which I have been doing. Now I’m back and I hope I will take my responsibility to give you out what young people the view through the window. So get prepared, thanks. By Isack 

Welcome to Youth Voice!

Follow this blog to hear from many different people every month. The youth of the world will send their views on politics, economics, society, the environment...anything! Tell us about what you've seen in the world. Tell us what you've heard. This blog will be for the youth to tell their stories from Alaska to Zanzibar!