Friday, March 29, 2013

Gorofa laanguka Dar es salaam

Leo wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameianza siku kwa majonzi makubwa baada ya taarifa za kuanguka kwa jengo la gorofa 16 katika eneo maarufu kwa msongamano wa watu na pilika pilika mbalimbali la kariakoo. Taarifa za awali zimemkariri Meya wa Ilala mheshimiwa Jerry Silaa kuwa maiti 2 zimepatikana na majeruhi 17. Pia muheshimiwa Silaa ameeleza kuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kusimamia zoezi la uokoaji na ulinzi wa mali za raia katika eneo hilo. YOUTH VOICE inaahidi kuwaletea habari kamili kadri zitakavyo kuwa zimapatikana na kuthibitiswa na vyombo vyenye mamlaka ya kutoa taarifa.

Tunapenda kutoa pole kwa watanzania wenzetu ambao wamewapoteza ndugu na marafiki zao, pia na wale waliopata majeraha wapone haraka. Pia tunaomba zoezi la uokoaji lifanyike kwa kasi na kwa uangalifu wa hari ya juu ili kuepusha madhara kwa watu ambao wanasadikika pengine wamefukiwa na kifusi hicho. Pia tunaomba hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote ambao kwa namna moja ama nyingine walikwepa majukumu yao ama kwa kukusudia au kuto kukusudia na kusababisha jengo hilo kupolomoka. Tumechosha na hii tabia ya vifo kwa watanzania wasio kuwa na hatia ambavyo husababiswa na uzembe wa watu katika majukukmu yao




                           


                                       


No comments:

Post a Comment


Welcome to Youth Voice!

Follow this blog to hear from many different people every month. The youth of the world will send their views on politics, economics, society, the environment...anything! Tell us about what you've seen in the world. Tell us what you've heard. This blog will be for the youth to tell their stories from Alaska to Zanzibar!