Jeshi la polisi Zanzibar linamshikilia mtu mmoja
alietambulika kwa jina la Omar Mussa Makame kwa tuhuma za mauaji ya Padri
Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar yaliotokea mwezi uliopita. Akizungumza na waandishi wa
habari mjini Zanzibar Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kuwa
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumekuja baada ya kutolewa kwa picha yenye sura ya
mtuhumiwa iliyochorwa na askari wa shirika la upelelezi la Marekani FBI.
Mtuhumiwa Omar Mussa Makame ambae ni mkazi wa Mtaa wa Raha Leo mjini Zanzibar alikamatwa na
kufanyiwa gwalide la utangulizi ambalo lilihusisha watu baadhi ambao walikuwepo
siku ya tukio ambao walitambua sura ya mtuhumiwa.
Akifafanua zaidi kamishina
Mussa Ali Mussa alisema kuwa jeshi la polisi litampatia zawadi ya million kumi
kwa siri mtu aliefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kama ilivyoahidi. Padri
Evarist Mushi aliuwawa Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada
katika kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Raas mjini Zanzibar.
Taswira ya mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Mushi kama ilivyoandaliwa na FBI
Gari la marehemu Padri Mushi muda mfupi baada ya ya kuuwawa kwa kupigwa risasi

No comments:
Post a Comment