Sakata la kumwagiwa tindikali mabinti wawili wa kiingereza ambao walikuwa wakijitolea huko Zanzibar rimechukua sura mpya baada ya watu mbalilmbali kutoa maoni ya kulaani tukio hilo. Wakitoa maoni yao kupitia mtandao wa skynews watu hao wamelaani na wengine kufikia hatua ya kumuomba waziri mkuu wa Uingereza kusitisha misaada kwa nchi ambazo ni tishio kwa raia wa nchi hiyo.
Akizungumza na skynews mama wa Kate Gee alisema kuwa mwanae ameungua sana na hivyo wanafanya jitihada kubwa ili aweze kulejeshwa nyumbani. Amesema familia kwa ujumla imesikitishwa sana na tukio hilo na kwasasa wanafanya uwezekano mtoto wao apate matibabu. tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kadri tunavyozipokea kutoka vyanzo vya habari vya uhakika
Mama wa Kate Gee
No comments:
Post a Comment