Friday, August 9, 2013

HATUKUZIBA UFA SASA TUNAJENGA UKUTA LO!!!!!!

Naomba kuchukua muda wangu kuzungumza na watanzania wenzangu ila kabla sijaeleza mengi kwanza ningeomba kuuliza je hii ndio Tanzania tuitakayo? Je watanzania huyu pepo wa kuua na kudhuru watu ametoka wapi? Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi sana ya kuhudhunisha na kushitusha kwa watanzania wote. Ilianza kama mzaha pale ambapo kiongozi mmoja wa dini alipomwagiwa tindikari huko Zanzibar.

Kama mdhaha matukio ya watu kumwagiwa tindikali yakazidi kusambaa kwa kasi na hivi karibuni mfanya biashara maarufu hapa nchini ambaye anahusika na kuudha vifaa vya majumbani katika moja ya maduka maarufu hapa Dar alipomwagiwa tindikari. Yapo mengi ambayo yanasemwa baada ya matukio kama haya kutokea ambapo watu huyahusisha na mambo mbalimbali kama visasi na kadhalika

Kwa kuudhibitisha usemi usemao kuwa usipoziba ufa utajenga tabia hii imewakumba hata wageni ambao ni watu waliokuja kujitolea kufundisha watanzania bure bila malipo. Watanzia walistuka baada ta taalifa za mabinti wawili raia wa Uingereza Kate Geee na Kirstie Trup kumwagiwa tindikari na watu wasio julikana


Hivi hawa watu waliofanya hili tukio ni watanzania au ni maadui zetu wa kibiashara (utarii), nakama ni watanzania wanalengo gani na taifa letu? Je Tanzania yetu kwli imefika hapa tulipo kwa kuwashambulia watu ambao wamekuja hapa nchini kwetu kujitolea kufundisha watanzania? Mimi natoa wito kwa watanzania, vyombo vya usalama na serikali kwa ujumla kushikamana kuwafichua hawa wanaotaka kutia doa sekta ya utarii. Wenzetu wa Tanzania Zanzibar wanategemea sana utalii katika kuongeza kipato cha wazanzibali na serikali kwa ujumla.

Hebu tushikamane pamoja kuwafuchua hawa na ile tabia ya vyombo vya usallama na serikali kusema upelelezi unaendelea kisha mnakaa kimya utatufikisha pabaya kama taifa.

No comments:

Post a Comment


Welcome to Youth Voice!

Follow this blog to hear from many different people every month. The youth of the world will send their views on politics, economics, society, the environment...anything! Tell us about what you've seen in the world. Tell us what you've heard. This blog will be for the youth to tell their stories from Alaska to Zanzibar!